Nilifanya project hii ya ku decorate rangi za ndani kwenye nyumba ya mteja Pugu.....
Pia tulifunga bomba za pazia vyumba vyote.....pamoja na kumtengenezea stand ya viatu na stand ya jikoni ya kuwekea vitunguu, nazi, mabilinganya, viazi, ndizi etc.......Nili provide consultation service...nikafanya colour selection kwa vyumba vyote vya ndani kwanzia sebuleni, dining room, jikoni, corridors, master bedroom, boys room, girls room, na bafuni.......baada ya hapo kazi ya kupaka rangi ikaendelea.
Baada ya zoezi la rangi kukamilika nikafunga bomba za pazia double kwa kuwekea pazia zito kwa mbele na pazia jepesi kwa nyuma...au shear curtain.... kwa madirisha ya vyumba vyote nyumba nzima.
Namshkuru Mungu niliweza kuikamilisha project hii na mteja wangu alifurahi sana.
.....ikiwa ungependa kupatiwa consultation service karibu sana Fancy Home Decor...Bado naendelea kutoa huduma hii.
Call us +255 0712 023102
|
Muonekano wa Corridor na sebule.. |
|
Rangi nilizo select tuka decorate sebuleni na dining room....muonekano wake kabla hatujafunga bomba za pazia. |
|
Dining room......kabla hatujaanza kufunga bomba za pazia |
|
Hapa ni corridor....nilichagua rangi hii tukupaka corridor ili kuifanya corridor iwe na mwanga na sio giza. |
|
Kwenye entrance ya kuingia Masterbedroom nili select rangi tofauti kidogo ila inayoendana na hiyo ya corridor... |
|
Rangi niliyopaka kwenye entrance ya kuingia masterbedroom.....iliendana pia na rangi niliyochagua tukapaka masterbedroom. |
|
Masterbedroom colour... |
|
Baby girls room....rangi ya pink ilitawala. |
|
Boys room.....nili select tukapaka rangi hizi |
|
Double Curtain rails, poles & holdbacks design......Muonekano wa boys room baada ya kufunga bomba za pazia kwenye madirisha. |
|
Double Curtain rails, poles & holdbacks design in masterbedroom.....Bomba za pazia nilizofunga kwenye madirisha ya masterbedroom. |
|
Nilifunga bomba 2 kwa ajili ya kuweka pazia zito kwa mbele na pazia jepesi au shear curtain kwa nyuma....na holdbacks za kushikia pazia kwa pembeni chini. |
|
Muonekano wa sebuleni baada ya kufunga bomba za pazia....curtain rails |
|
Hapa ni jikoni......hapa napo pia tulipaka rangi hiyo kwa juu ya tiles....then nikafunga bomba za pazia....Single Curtain rails & poles.... |
|
Dirisha la bafuni nalo tukaweka bomba la pazia...na kwa juu tukapaka hiyo rangi |
|
Rangi niliyo select tukapaka kwenye Entrance room ya kuingia bafuni/chooni.... |
|
Mwisho kabisa nikatengeneza na ku deliver hii shoe rack ya ngazi 7.... |
|
Hii stand nayo nili deliver....ni stand ya jikoni ya kuwekea vitunguu, nyanya, viazi, mabilinganya, nazi, ndizi, matunda etc..... |