Saturday, July 13, 2013

MY PROJECT: ROCK WATERFALLS DESIGNING & DECORATION - BEFORE & AFTER - SITE YA MAKONGO

DESIGNER: MERCY - FANCY HOME DECOR

PROJECT: EXTERIOR ROCK WATERFALLS DESIGNING & DECOR

LOCATION: MAKONGO JUU

CONTACT: 0712 023102Namshkuru Mungu kwa kuniwezesha kuifanya na kuimaliza salama project hii ya ku design na kupaka rangi nje ya nyumba, kwenye maporomoko ya mawe yaliyokwisha kujengwa kwa kuizunguka fence ya nyumba huko Makongo juu. 

Tayari mteja wangu alikwisha kuyajenga na kuweka pump ya maji ili kusababisha "waterfalls" view au maji kutiririka kuingia kwenye pool ambayo nayo iliipakwa rangi yake.Kitakachofuata baada ya hapa ni gardening. Kutapandwa "plants" au maua maalumu mazuri kwenye sehemu ya mawe zilizojazwa udongo tayari. Hii ni kazi ya sanaa na kiubunifu zaidi.

Ni kweli baadhi yetu tumezoea kuona design hizi za "rock waterfalls" kwenye mahoteli makubwa... lakini hii ni kazi ya ubunifu inayoweza kujengwa katika nyumba zetu ambapo kama ukifanyiwa kazi kitaalamu lazima nyumba zetu zitavutia sana. 
Na sio nje tu ya nyumba yako...bali mawe haya unaweza kuyajenga hata ndani ya nyumba yako mfano; sebuleni, na kuyapaka rangi nzuri zitakazoshahabiana vyema.

Usisubiri kusimuliwa, anza sasa kufikiria kujenga rocks waterfalls kama hii nyumbani kwako. Embu angalia inavyovutia.BEFORE


The rocks are built at a front yard of the house...Mawe haya yamejengwa kuuzunguka ukuta wa nje ya   nyumba kama mnavyoona hapa. 

                                       gogo lililojengwa kiubunifu na ustadi kwa kutumia cement
                                A creative work of rocks waterfalls design...so unique and amazing !
                                      Mawe yamejengwa kwa ubunifu wa hali ya juu...                                                    

                               Water pool surrounded by small beautifull decorative stones...
  Hichi ndo kisima kwa ajili ya maji yanayotiririka kutuama. Kimezungukwa na mawe ya tarazo yenye rangi  mchanganyiko.
AFTER
                                Pool ya maji ikiwa tayari imeshapakwa rangi yake...beautiful view


                        Hapa patakuja kufanyiwa "gardening...mawe mazuri yanayoizunguka ni ya tarazo


   Gogo linaloonekana limefanyiwa decoration ya rangi  nzuri inayoongezea mvuto kwenye macho


                     Mvuto wa rangi zilizochangwanywa kiubunifu kwenye gogo na ukuta...inapendeza

                        
                                                              Inapendezaa kwakweli...


Dear visitor, r u inspired?....
Rock waterfalls is the hottest trendy exterior decor and design for home owners. It brings a beautiful view especially at the front yard of your house or at the backyard and at your garden.
You should try this at your home.

Lets Decorate, Relax, Live & Enjoy.


*Shukrani za dhati pia ziende kwa mteja wangu... Nashkuru kwa kuniamini na kwa kuifurahia kazi yangu hii. Mbarikiwe sana.*


 
Related Posts Plugin for Blogger...